Kikosi cha Yanga jana kilifanya mazoezi yake kwenye uwanja wa New Amaan Complex yakiwa ni maandalizi kulekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger.
Mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Novemba 28 utapigwa kwenye uwanja huo.
Yanga ilirejea Zanzibar tangu Jumanne ikijiandaa na mtanange huo ambao Wananchi wamepamia kuondoka na alama tatu.
Timu ya MC Alger tayari imewasili visiwani Zanzibar jana jioni ambapo leo itapata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja huo.
Ikumbukwe kesho Ijumaa dimba la New Amaan Complex utachezwa mchezo wa kombe la Shirikisho (CAFCC) kati ya Azam Fc dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.







