Klabu ya Yanga imetangaza kuachana rasmi na kiungo wake mkabaji Justine Zulu 'Mkata Umeme' aliyesajiliwa miezi nane iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Charles Mkwasa amesema Yanga iko kwenye mchakato wa kumlipa stahiki zake baada ya kuvunja mkataba wake.
Mkataba wa Zulu unamaliza mwezi Novemba mwaka huu lakini ni dhahiri kushindwa kwake kudhihirisha ubora wake kwenye kikosi cha Yanga, ilikuwa ni lazima kwa uongozi uachane nae.

ADVERTISE HERE