Mkemi azishukia Vodacom, TFF na Bodi ya ligi

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
4 Aug 2017
Mkemi azishukia Vodacom, TFF na Bodi ya ligi
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga, Salum Mkemi ameitaka kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom ambayo ndiyo wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania Bara kuiomba radhi Yanga kwa kitendo cha kutoialika kwenye hafla ya kugawa vifaa vya michezo kwa vilabu vitakavyoshiriki VPL msimu huu.

Mkemi pia amelitaka shirikisho la soka nchini (TFF) na Bodi ya ligi kuomba radhi kwa maandishi kufuatia tukio hilo lisilo la kiungwana.

Aidha Mkemi amelaani kitendo kilichofanywa na Afisa Habari wa Klabu ya Simba Haji Manara eti kuiwakilisha Yanga kupokea vifaa vyake na kisha kutumia tukio hilo kuikejeli klabu hiyo kongwe zaidi nchini Tanzania.

"Yanga ndiyo timu yenye mafanikio zaidi nchini Tanzania. Tumetwaa taji la ligi kuu ya Vodacom kwa misimu mitatu mfululizo," amesema Mkemi.

"Pia Yanga imetwaa mataji saba ya ligi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Yanga imetwaa taji la ligi kwa jumla mara 27"

"Hawakupaswa kutufanyia kitendo hichi cha kuidhalilisha timu ambayo ndio mabingwa watetezi wa ligi."

Aidha Mkemi amekwenda mbali zaidi kwa kuhusisha kitendo hicho kuwa ni cha kuhujumu mapato ya klabu ya Yanga.

"Yanga ilipanga siku maalumu ya kutambulisha jezi yake. Sasa kitendo tulichofanyiwa ni hujuma kwani kwa kitendo cha wao kuonyesha jezi yetu jana wamepelekea tukio hilo kutokuwa na maana," amesema.

Mkemi pia amefafanua kuwa jezi hizo sio mali ya Vodacom, jezi za Yanga zimetolewa na kampuni ya SportPesa, ameitaka kampuni ya Vodacom kuacha kupotosha UMMA kwa kudai kuwa wameipa jezi klabu ya Yanga.

Mkemi ameishukia Bodi ya Ligi kwa kuweka ushabiki katika tukio hilo ambalo anaamini liliandaliwa na 'wanazi' wa Simba wengi walio kwenye Bodi hiyo.

"Walipanga kutudhalilisha makusudi, sasa tunawataka watuombe radhi kabla hatujachukua hatua zaidi."

Kwa muhjibu wa Mkemi, jezi za Yanga zingezinduliwa kwenye tukio maalumu ambalo lingeongozwa na mlinzi wa zamani wa Arsenal Sol Campbell.

"Jezi zilikuwa zitambulishwe na Soul Campbel na Sportpesa waliingia mkataba na kampuni ya Joma, jezi hizo zimetambulishwa kihuni na Vodacom na Haji Manara," amesema.

Amesema Yanga inajipanga kuchukua hatua kwa tukio hilo la kutolewa jezi yake hadharani bila kushirikishwa tena likiharibu mipango yake ya kibiashara.

Mkemi amemshukia Kassimu Dewji anayemiliki duka lililokuwa limepewa kazi ya kuweka nembo ya SportPesa katika jezi za Yanga.

Amemtaka aombe radhi kwa kitendo chake cha kuzikabidhi jezi hizo kwa Vodacom licha ya kujua jezi hazikuwa mali yao.

Aidha katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa ameitaka TFF iziache klabu zilipe kodi ya mapato (VAT) zenyewe badala ya kuzikata pesa hizo.

Mkwasa amesema klabu zote zina akaunti TRA kwa ajili ya kulipia VAT lakini cha kushangaza TFF imekuwa ikizikata klabu VAT na kuwasilisha pesa hizo kwa niaba ya vilabu.

Ameitaka Mamlaka ya mapato, TRA itoe elimu kwa vilabu juu ya mkanganyiko huo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’