Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema klabu hiyo imejikita katika kusajili wachezaji wanaoweza kutumika kwa muda mrefu.
Nyika amesisitiza kuwa Yanga haikuwahi kuwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji Medie Kagere aliyesajiliwa na Simba kwa kuwa licha ya ubora wake, hana moja ya vigezo muhimu wanavyohitaji.
"Kagere ni mchezaji mzuri naheshimu uwezo wake, lakini sisi hatukuwahi kuwa na mpango wa kumsajili kwa kuwa aina ya wachezaji tunaowataka ni wale ambao tunaweza kuwatumia kwa muda mrefu, angalau miaka mitatu," amesema Nyika.
Moja ya sababu inayoifanya Yanga iwe na mafanikio zaidi ni utaratibu wao wa kuwa na vikosi vinavyodumu.
Kikosi cha Yanga kilichotwaa mataji matatu ya VPL mfululizo hakikuwa na mabadiliko makubwa kabla ya msimu uliopita timu hiyo ilipoingiza damu changa.

ADVERTISE HERE