Hakuna adhabu kwa Yanga baada ya kujitoa Kagame Cup

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jun 2018
Hakuna adhabu kwa Yanga baada ya kujitoa Kagame Cup
Shirikisho la vyama vya soka Afrika Mashariki na kati (CECAFA) limesema klabu ya Yanga haitaadhibiwa baada ya kujitoa katika michuano ya klabu bingwa Afrika ya Mashariki na Kati inayotambuliwa kama CECAFA Kagame Cup.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Makao Makuu ya TFF, Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye amesema mabingwa hao wa Tanzania Bara msimu wa 2016/17 wamejitoa kutokana na sababu zao na wao hawana pingamizi.

Musonye amesema anaitakia kila la kheri Yanga katika maandalizi yake ya michuano ya kombe la Shirikisho na kuiombea ifike mpaka fainali.

"Mimi siko hapa kusema mambo mabaya leo. Yanga wametoa sababu zilizopelekea washindwe kushiriki mashindano haya. Tumewakubalia na tunawatakia kila la kheri katika maandalizi yao," amesema Musonye.

Michuano ya CECAFA Kagame Cup inaanza kesho Ijumaa jijini Dar es salaam.

Yanga ilijitoa katika michuano hiyo sababu kubwa ikitajwa ni kuwapa mapumziko wachezaji wake huku ikielezwa pia kuwa na idadi kubwa ya wachezaji ambao hawana mikataba.

Vilabu vya Rayon Sports na Gor Mahia ambavyo viko kundi moja na Yanga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho, vitashiriki michuano hiyo.

Hata hivyo timu hizo zimetangaza kutumia vikosi vyao vya pili kushiriki mashindano hayo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’