Baada ya mapumziko ya siku moja, michuano ya kombe la dunia inayofanyika nchini Urusi inaendelea leo ambapo michezo miwili kati ya nane ya hatua ya mtoano itapigwa.
Saa 11 jioni Argentina itakuwa na kibarua kigumu pale itakapoikabili Ufaransa.
Wakati Ufaransa ikifanikiwa kutinga hatua ya mtoano bila kupoteza mchezo, Argentina ilihitaji muujiza wa Lionel Messi kuweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Nigeria.
Argentina haipewi nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na ukweli kwamba imekuwa ikimtegemea zaidi Messi wakati Ufaransa ina wachezaji wengi wanaoweza kuipa matokeo wakati wowote.
Wachezaji tisa wako hatarini kuukosa mchezo wa robo fainali kama timu zao zitafuzu iwapo wataonyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo huo.
Kwa upande wa Ufaransa ni Corentin Tolisso, Paul Pogba, Blaise Matuidi wakati Argentina walio hatarini ni Gabriel Mercado, Nicolas Otamendi, Marcos Acuna, Javier Mascherano, Ever Banega na Lionel Messi.
Saa tatu usiku kutakuwa na mchezo mwingine wa kukata na shoka kati ya Uruguay dhidi ya Ureno.
Uruguay imetinga hatua ya mtoano ikiwa vinara wa kundi A baada ya kushinda michezo yake yote mitatu wakati Ureno ilipenya 'kimagumashi' katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Iran.
Matokeo ya Ureno yatategemea zaidi hali ya kimchezo ya mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo.
Mkali huyo wa mabao anayekipiga na Real Madrid ameifungia timu hiyo mabao manne akiwa nyuma kwa bao moja dhidi ya kinara wa mabao kwenye michuano hiyo Harry Kane wa Uingereza.
Uruguay itawategemea washambuliaji wake Luis Suarez na Edson Cavan. Suarez amefunga mabao mawili kwenye michuano hiyo wakati Cavan amefunga bao moja.
Rodrigo Bentancur wa Uruguay, Bruno Fernandes, Adrien Silva, Raphael Guerreiro, Ricardo Quaresma, Cristiano Ronaldo na Cedric wote wa Ureno wanaweza kukosa mchezo wa robo fainali kama wataonyeshwa kadi za njano.
Kama Argetina na Ureno zote zitafuzu zitakutana kwenye mchezo wa robo fainali.

ADVERTISE HERE