Kocha Mkuu wa Yanga Zahera Mwinyi ameendelea kukinoa kikosi chake viwanja vya chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam.
Mbali na kuendelea na zoezi la kuwajaribu baadhi ya wachezaji, Zahera ameendelea na program kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa baadae mwezi huu nchini Kenya.
Yanga imeendelea kuleta wachezaji wapya kuwajaribu kwa ajili ya kuwasajili kama watafuzu majaribio hayo.
Baada ya kuondoka kwa Marcellin Koukpo, uongozi wa Yanga umemleta mshambuliaji mwingine kutoka Nigeria, Emeka Emarun (23).

Emarun ametokea klabu ya FK Radnick Pirot inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Serbia.
Licha ya kucheza kama mshambuliaji wa kati, Emarun anaweza kucheza wingi zote.
Mshambuliaji huyo pia amewahi kucheza katika vilabu vya Bayern Munich (U19), Bizerte (Tunisia) na Esperance (Tunisia)
Ujio wake unadaiwa kufanikishwa na kocha Mwinyi Zahera kwa kushirikiana na Kamati Maalum inayoongozwa na Tarimba Abbas.

ADVERTISE HERE