Aliyewahi kuwa Katibu wa Mipango wa Klabu ya Yanga Abdul Sauko amesema winga Mrisho Ngassa amerejea nyumbani katika klabu ya maisha yake.
Ngassa alianza kujifua kwenye kikosi cha Yanga jana baada ya kumalizana na uongozi wa timu hiyo.
"Ngassa ni kijana wetu, tulimpokea Yanga akiwa mdogo wakati huo akitokea Kagera Sugar. Amepata mafanikio zaidi ya soka akiwa katika klabu ya Yanga hivyo ni kama amerejea nyumbani," Sauko ameiambia EFM Radio.
Sauko pia amewashangaa wale wanaobeza usajili huo wakidai Yanga imemsajili Ngassa kwa kuwa haina uwezo wa kifedha wakati huu.
"Kuna timu zinazodaiwa kuwa na fedha zimesajili wachezaji ambao walishindwa hapa nchini, wakaenda nje ya nchi wakashindwa lakini wamewachukua."
"Lakini kwa umri wake Ngassa bado ana miaka zaidi kung'ara pengine kuliko hata baadhi ya wachezaji wakongwe waliosajiliwa na timu nyingine kwa mbwembwe"
Ngassa mwenye umri wa miaka 29 anatabiriwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na Yanga ambao wataweza kurejesha makali ya mabingwa hao wa kihistoria Tanzania Bara

ADVERTISE HERE