Straika Mnigeria wa Yanga afichua alivyotua Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
3 Jul 2018
Straika Mnigeria wa Yanga afichua alivyotua Tanzania
Straika mpya Mnigeria aliyetua usiku wa juzi Jumapili akitokea Serbia, Emeka Emerun Jacobs, leo Jumanne anaweza akaanza kazi pale Yanga, lakini jamaa ametamka kwamba hataki kuongea mengi juu ya ubora wake akitaka mashabiki wamsubiri uwanjani, huku akifichua namna mabosi wa Jangwani walivyomfanyia umafia katika safari yake ya kuja Tanzania.

Emeka alisema amekuja Tanzania kucheza soka na ubora wake utaonekana uwanjani, iwapo tu atakamalizana na mabosi wa Yanga ambao alifichua namna walivyotumia akili nyingi kumshusha nchini ili kuzungumza naye kwa lengo la kumsajili.

Emeka amesema ubora wa kipaji chake ni kwamba ana ujuzi wa majukumu mawili ya kujua kutengeneza mabao na hata kufunga kazi ambazo hana mashaka nazo.

Mnigeria huyo alisema mbali ya hayo endapo atamalizana na mabosi wa Yanga ni kwamba anaweza kutoa huduma katika nafasi tano uwanjani kwa kumudu kucheza nafasi zote hizo akizitaja kuwa ni winga wa kulia au kushoto, nafasi za mastraika wa kati na hata kiungo mchezeshaji.

“Sitaki niwe muongeaji sana kuhusu hilo swali la ubora wangu, nafikiri acha mambo yakazungumze uwanjani, ila ninapokuwa uwanjani kazi yangu itapimwa kwa kutengeneza nafasi za timu yangu kupata mabao na kufunga, hayo ndiyo ninayoyajua,” Emeka ameliambia Mwanaspoti

“Ninamudu kucheza nafasi zisizopungua nne uwanjani, naweza kucheza wingi ya kulia na kushoto, pia nafasi za ushambuliaji za kati na kama ikitokea kuna uhaba wa kiungo naweza kucheza kiungo mchezeshaji,” alisema.

“Kocha ataamua kunipa jukumu gani, mimi ni mchezaji kazi yangu ni kuwa tayari na majukumu ninayotakiwa kuyatekeleza kucheza nafasi zote hizo ni kutokana na kubahatika kujua vyema kutumia miguu yote sawasawa.”

Mchezaji huyo aliyewahi kuzichezea FK Radnick Pirot ya Serbia amefichua kwamba awali alikuwa anajiandaa kwenda Afrika Kusini, lakini ghafla meneja wake alimtaarifu kwamba safari yake imebadilika na kwamba Yanga imeinunua safari hiyo.

Emeka alisema alidokezwa watu wa Kamati ya Usajili wa Yanga, waliinunua safari hiyo juu kwa juu ili atue Dar es Salaam na kufanya akanyage Tanzania bila kutarajia kwani hakuwahi kufikiria kuja kucheza hapa.

“Mpaka sasa siamini kama niko hapa Tanzania, mpaka Ijumaa wiki iliyopita nilikuwa najua naenda Afrika Kusini kuna timu tatu zilikuwa zikinihitaji, angalia mpaka visa nilishapata

“Meneja wangu akanifuata usiku wa siku hiyo akaniambia safari hiyo haitaweza kukamilika tena kwa vile kuna timu imenunua na kugharamia kila kitu wanataka nije Tanzania kila kitu kilifanyika kwa haraka sana ndio mpaka sasa unaniona hapa," alisema Emeka.

“Nafikiri hao viongozi walionileta hapa ndiyo wenye bahati sana, sikuwa najua kama ningekuja huku Tanzania ingawa ni nchi ninayoisikia kwa muda mrefu lakini sijui lolote kuhusu soka la hapa,” alisema Emeka ambaye alifichua kupoteza begi lake safarini.

“Lakini katika soka hakuna ugeni.”

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →