Mchakato wa Mabadiliko usicheleweshwe Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jul 2018
Mchakato wa Mabadiliko usicheleweshwe Yanga
Njia pekee ya Yanga kujiimarisha kiuchumi ni kuingia katika mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ambayo tayari yameridhiwa na wanachama wa klabu hiyo.

Tangu kuondoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wake Yusuf Manji, Yanga imekumbwa na wakati mgumu wa kiuchumi.

Kumekuwa na jitihada za kumrejesha Manji katika nafasi ya Uwenyekiti baada ya wanachama kuikataa barua yake ya kujiuzulu lakini karibu mwezi sasa Manji amekuwa kimya.

Yanga ililazimika kuunda Kamati Maalum ya Mpito kusaka fedha ili iweze kufanya usajili wakati huu.

Nadhani ni wakati muafaka kwa Yanga kuachana na utaratibu wa kuendesha klabu kwa kutegemea mtu mmoja.

Moja ya changamoto inayodaiwa kuikwamisha Yanga kufanya usajili wake kwa wakati mwaka huu ni kukosekana kwa fedha.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Hussein Nyika alikiri kuwa usajili wa Yanga unafanywa kulingana na fungu linalowasilishwa na Kamati Maalum ya klabu hiyo inayoongozwa na Abbas Tarimba.

Wakati huu hakuna tajiri anayetoa pesa yake kufanya usajili kama ilivyokuwa wakati wa Manji.

Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana Yanga iliunda Kamati ya Mabadiliko inayoongozwa na Mwanasheria Alex Mgongolwa.

Hata hivyo tayari imepita zaidi ya miezi sita bila ya Wanachama wa Yanga kupewa mrejesho juu ya nini kinaendelea.

Mapema leo wakati akihojiwa na EFM, Mgongolwa alisema tayari Kamati yake imemaliza kazi iliyopewa ya kupendekeza mfumo bora wa uendeshaji na wanatarajia kuwasilisha mapendekezo hayo kwa Kamati ya Utendaji hivi karibuni.

Mgongolwa amesema Kamati yake imependekeza mfumo wa hisa kupitia kampuni ambayo wanachama wataimiliki kwa asilimia 51 na wawekezaji asilimia 49.

Wakati huu ambao Yanga inapita katika kipindi kigumu ndio wakati wa kuharakisha michakato hiyo ili klabu iweze kujitegemea.

Hakuna shaka mchakato huo ukikamilika, watajitokeza WanaYanga wengi kununua hisa na huo utakuwa mwanzo wa Yanga imara.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’