Leo ndio Yanga imekabidhi rasmi jezi na wadhamini, Kampuni ya Sportpesa leo.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas aliikabidhi Yanga jezi hizo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya mchezo dhidi ya Singida United.
Akizungumza wakati wa kukabidhi jezi hizo, Tarimba alisema imefika wakati jezi za klabu hiyo kuanza kuheshimiwa huku akitoa ushauri kwa klabu kuanza kutumia jezi zao kama moja ya vitega uchumi.
"Jezi ni kitu kikubwa mno kwenye timu ndiyo sababu SportPesa tunalaani tukio lililotokea hivi karibuni wakati timu zikikabidhiwa jezi tena ikatokea vitendo vya kubeza.
"Jezi za Yanga zilizoonyeshwa kwenye tukio hilo sisi (SportPesa) tulizipeleka kwenye printing, lakini tukashangazwa kuonyeshwa kule," alisema Tarimba baada ya kukabidhi jezi huku vifaa vingine akieleza vitakabidhiwa kwa timu huska.
Akipokea jezi hizo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi alisema jezi walizokabidhiwa zinakiwango na kusisitiza wanaandaa utaratibu maalumu kwa ajili ya jezi zao original kuanza kuuzwa na klabu kunufaika na mauzo hayo.

ADVERTISE HERE