Yanga kutii agizo la Serikali, kuitisha uchaguzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jul 2018
Yanga kutii agizo la Serikali, kuitisha uchaguzi
Uongozi wa Yanga uko mbioni kutii agizo la Serikali kwa kuitisha uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi.

Katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu hiyo uliofanyika Juni 10, 2018 jijini Dar es salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe aliupa uongozi wa Yanga siku 60 kuziba nafasi zilizowazi kwa mujibu wa Katiba ya timu hiyo.

Jana katika Mkutano wa Wenyeviti wa matawi wa klabu ya Yanga, Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga alisema wanajiandaa kuwaandikia barua TFF kuwajulisha kuwa sasa wako tayari kufanya uchaguzi wa nafasi zilizo wazi.

Nafasi zilizowazi ni nafasi mbili za wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Manji anarudi

Wakati huo huo Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amethibitisha kuwa Yusufu Manji, ameridhia kurejea klabuni hapo.

Kufuatia uamuzi wa Wanachama wa Yanga kupitia Mkutano Mkuu, kuikataa barua ya kujiuzulu kwa Manji, uongozi wa Yanga ulimtaarifu bilionea huyo uamuzi wa wanachama na tayari Manji ametoa majibu.

Sanga amesema kuwa Manji amewashukuru wanachama kwa kuendelea kuwa na imani naye hivyo ameomba muda wa angalau miezi miwili au mitatu ili aweze kukamilisha mambo yake kabla ya kurejea rasmi klabuni.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’