Yanga inaiwinda Gor Mahia kimyakimya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jul 2018
Yanga inaiwinda Gor Mahia kimyakimya
Yanga imeendelea kujifua kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa Jumatano ijayo, Julai 18, Nairobi Kenya.

Gor Mahia bado iko nchini ambapo jana ilitinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Kagame kwa kuilaza Vipers Fc mabao 2-1.

Uwepo wa timu hiyo hapa nchini umelipa nafasi benchi la Ufundi la Yanga kuwasoma na kubaini madhaifu yao kuelekea mchezo baina ya timu hizo.

Baada ya kukamilisha zoezi la majaribio kwa baadhi ya wachezaji, Yanga sasa imejikita zaidi katika maandalizi kuelekea mchezo huo.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema anakiandaa kikosi chake kikamilifu kuhakikisha hakipotezi mchezo huo wa ugenini nchini Kenya.

Aidha ujio wa Mrisho Ngassa, Deus Kaseke na Haritier Makambo kwenye kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya CAF, umeimarisha makali ya safu ya ushambuliaji.

Yanga bado ina nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo kama haitapoteza michezo yake miwili ya ugenini dhidi ya Gor Mahia na Rayon Sports na kushinda michezo yake yote ya nyumbani dhidi ya Gor Mahia na USM Alger.

Ratiba ya michuano hiyo inaonyesha baada ya mchezo dhidi ya Gor Mahia Julai 18, Yanga itarudiana tena na Gor Mahia jijini Dar es salaam Julai 29.

Agosti 19 itawakaribisha USM Alger kwenye uwanja wa Taifa kabla ya kusafiri nchini Rwanda kumaliza mchezo wa mwisho dhidi ya Rayon Sports Agosti 29.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’