Dirisha kubwa la usajili linafungwa leo, Agosti 06 saa sita usiku. Wakati huu Yanga pamoja na timu nyingine ziko 'busy' kumalizia zoezi hilo.
TFF ilishatahadharisha kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa timu zitakazoshindwa kukamilisha zoezi hilo kwa wakati kwani ni FIFA wanaofunga utaratibu.
Yanga ilishakamilisha usajili wake kwa asilimia 90 kulingana na taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Charles Mkwasa, katika hizo asilimia 10 zilizobaki jana ameongezwa Gadiel Michael.
Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji 24 na kocha Lwandamina anataka kikosi cha wachezaji angalau 25. Kiwango cha juu kinachoruhusiwa ni wachezaji 30 ambapo wachezaji 7 wanaweza kuwa wa Kimataifa.
Tutarajie mambo mazuri muda mfupi ujao, Kamati ya usajili ya Yanga iko makini wakati huu pengine kuliko wakati mwingine wowote.

ADVERTISE HERE