Yanayojiri Urusi : Ufaransa na Ubelgiji nusu fainali kombe la dunia leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Ufaransa na Ubelgiji nusu fainali kombe la dunia leo
Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia kati ya Ufaransa dhidi ya Ubelgiji unapigwa leo Jumanne, Julai 10 2018, saa tatu usiku kwenye dimba la Saint Petersburg.

Mchezo huo unazikutanisha timu mbili ambazo mojawapo inapewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe la dunia Jumamosi ijayo.

Timu hizo zimekutana mara 74 kwenye michuano mbalimbali Ufaransa ikishinda mara 24 huku Ubelgiji ikiibuka na ushindi mara 30 zikitoka sare mara 19.

Mara ya mwisho kukutana kwenye michuano ya kombe la dunia ilikuwa mwaka 1986 ambapo Ufaransa ilishinda kwa mabao 4-2 katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Ufaransa haijawahi kupoteza mchezo dhidi ya Ubelgiji kwenye michuano ya kombe la dunia ikishinda 3-1 kwenye mchezo wa kwanza zilipokutana mwaka 1938.

Wakati huu timu zote ziko katika viwango bora kabisa zikifanikiwa kutinga hatua hiyo kwa kuziondoa timu vigogo.

Hii ni mara ya pili kwa Ubelgiji ambayo haijawahi kutwaa kombe la dunia kucheza mchezo wa nusu fainali.

Ufaransa ilifanikiwa zaidi mwaka 1998 ilipotwaa taji hilo.

Inasaka rekodi nyingine ya kusinda taji hilo baada ya kupita miaka 20 huku sasa ikinolewa na Didier Deschamps ambaye alikuwa nahodha wa kikosi kilichotwaa ubingwa mwaka 1998.

Lakini Kocha Msaidizi wa Ubelgiji ni Thiery Henry ambaye naye alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa mwaka 1998 wakati huu akiwa najukumu la kumsaidia Roberto Martinez kuipeleka fainali Ubelgiji.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’