Juma Abdul amewapania kwelikweli Gor Mahia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
10 Jul 2018
Juma Abdul amewapania kwelikweli Gor Mahia
Beki wa Yanga, Juma Abdul, amejiunga na kikosi chake baada ya kumalizana na mabosi wake huku akichimba mkwara mzito kwa Gor Mahia ya Kenya kwamba wajiandae tu kisaikolojia katika pambano lao litakalopigwa Jumatano ijayo huko Kenya.

Yanga itacheza na Gor katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika na Abdul amesema pamoja na kuchelewa kujiunga na kikosi hicho kutokana na changamoto ya mkataba, lakini alikuwa akifanya mazoezi ya peke yake ili kujiweka sawa.

Alisema anaamini kuelekea kwenye mchezo huo mgumu wa Kundi D hawatafanya makosa kwani kikosi chao hakina mabadiliko makubwa kutokana na usajili wao walioufanya.

“Mkataba wangu ulimalizika na sasa nimemalizana na viongozi wangu juu ya mkataba mpya, nimerudi na nitatumia muda huu mchache uliobaki kuongeza uzoefu na kujifunza mbinu mpya ya mwalimu kwa lengo la kuhakikisha nafanya vizuri zaidi,” alisema beki huyo.

“Kitu kikubwa ninachoweza kusema ni kuwatoa wasiwasi mashabiki wetu, Yanga ni timu kubwa kwahiyo hata kama imefanya vibaya katika ligi tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, kikubwa kwa sasa ni kujipanga kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri tushirikiane kwa pamoja kuleta ushindi. Hii ni timu ya ushindi.”

Kwenye michuano hiyo ya kimataifa, Yanga inaburuza mkia katika kundi lake ikiwa na alama moja nyuma ya vinara USM Alger ya Algeria wenye alama nne, Gor Mahia na Rayon Sports ya Rwanda zinafuatia zikiwa na alama mbili kila moja.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →