Kuna taarifa kuwa Shirikisho la soka nchini (TFF) liko mbioni kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka saba hadi kumi watakaoruhusiwa kusajiliwa na timu katika dirisha la usajili la mwaka huu linalofungwa Julai 26.
Kulingana na taarifa iliyoripotiwa na baadhi ya magazeti leo, tayari TFF imevipa taarifa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom juu ya mabadiliko hayo.
Imeelezwa lengo la mpango huo ni kuzipa nguvu zaidi timu hasa zinazoshiriki michuano ya CAF (Klabu bingwa na Shirikisho).
Bado TFF haijatoa taarifa rasmi juu ya ukweli wa mpango huo.
Miaka ya nyuma utaratibu huo wa kusajili wachezaji 10 wa kigeni ulikuwepo lakini uliondolewa kwa lengo la kuwanufaisha wachezaji wazawa.
Pia mpango huo unaweza kuwa na athari ya moja kwa moja kwa timu ya Taifa kama hautaundiwa kanuni itakayotamka idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoruhusiwa kucheza kwenye mchezo mmoja.

ADVERTISE HERE