Shirikisho la soka nchini (TFF) limemsimamisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Clement Sanga baada ya kukosa sifa.
Uamuzi wa kumsimamisha Sanga umekuja kufuatia klabu ya Yanga kumrejesha kwenye nafasi yake Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji hivyo kumfanya Sanga akose sifa ya kuongoza Bodi ya Ligi.
Mapendekezo ya kumsimamisha Sanga yametolewa na Kamati ya Sheria na Katiba ya TFF.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo, Rais wa TFF Wallace Karia amesema kwamba hatua hiyo imefuatia baada ya uamuzi wa wanachama wa Yanga kupitia Mkutano wao Mkuu uliofanyika Juni 10, kumrejesha madarakani Yusufu Manji
Karia amesema sifa kuu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi ni lazima uwe Mwenyekiti wa klabu ya Ligi Kuu.
Sanga amepoteza sifa kwa kuwa sio Mwenyekiti wa klabu ya Yanga.
"Tulipokea barua June 12 kutoka klabu ya Yanga ikielekeza kuwa Sanga hatambuliki kama Mwenyekiti wa klabu hiyo.
"Wao Yanga wanamtambua Yussuf Manji ndiye Mwenyekiti wa klabu hiyo na katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi unatakiwa Uwe Mwenyekiti wa klabu yako," amesema Karia

ADVERTISE HERE