JKU yaikana Singida United usajili wa Fei Toto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2018
JKU yaikana Singida United usajili wa Fei Toto
Uongozi wa JKU umeikana klabu ya Singida United ambayo mapema leo ilitangaza kukamilisha usajili wa kiungo Feisal Salum 'Fei Toto'.

Meneja wa timu hiyo Mohammed Kombo Hamad amesema kitendo cha Singida United kutangaza kumsajili Fei toto ni kinyume na utaratibu kwa kuwa mchezaji huyo bado alikuwa na mkataba na JKU.

Hamad ameitaka TFF na vyombo husika kuichukulia hatua za kisheria Singida United kwa kutangaza kumsajili mchezaji anayemilikiwa kihalali na timu nyingine.

Hamad ambaye aliiwakilisha JKU wakati Feisal akitambulishwa kutua Yanga, amesema klabu ya JKU imemruhusu Feisal kusajiliwa na Yanga baada ya mabingwa hao wa kihistoria Tanzania Bara kukamilisha taratibu zote.

"Singida United hawakuwahi kuwasiliana nasi, tulisikia kwenye vyombo vya habari kuwa wamemsajili mchezaji wetu ambaye bado ana mkataba wa miaka miwili," amesema Hamad.

"Tuliwatahadharisha juu ya mpango wao huo kwa kuwaeleza kuwa Feisal bado ni mchezaji wetu halali, msimu uliopita alisaini mkataba wa miaka mitatu."

"Viongozi wa Yanga wamekuja mezani tumekubaliana, ndio maana tumewaruhusu wamsajili."
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’