Kessy mguu nje mguu ndani Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2018
Kessy mguu nje mguu ndani Yanga
Walinzi Hassani Kessy na Kelvin Yondani hawakusafiri na kikosi cha Yanga kilichokwenda Kenya kucheza na Gor Mahia mchezo wa kombe la Shirikisho.

Kessy na Yondani wameweka ngumu wakishinikiza wapewe 'mkwanja' kwanza ili waweze kusaini mikataba mipya.

Imeelezwa uongozi wa Yanga tayari ulishamalizana na Kelvin Yondani kinachosubiriwa ni kukabidhiwa fedha za usajili ili aweze kusaini mkataba mpya.

Lakini hali ni tofauti kwa Kessy ambaye pia anawaniwa na klabu ya Nkana FC ya nchini Zambia.

Wazambia hao wanataka kumsajili Kessy kwa dau la dola 35,000.

Mlinzi huyo wa pembeni aliyeng'ara msimu uliopita katika kikosi cha Yanga na kuingia kwenye kikosi bora cha msimu, ametaka dau la usajili la Mil 70 ili aweze kubaki Yanga.

Inadaiwa mabosi wa Kamati ya usajili ya Yanga wamegomea kiasi hicho cha pesa alichotaka Kessy na kama hakutakuwa na mwafaka kwenye majadiliano yanayoendelea, huenda beki huyo aliyetua Yanga kutoka Simba misimu miwili iliyopita akaruhusiwa aondoke.

Inaelezwa tayari Yanga imeanza kusaka mbadala wake ikitokea mwafaka haukufikiwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’