Yanga imeendeleza uteja katika michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kulazwa mabao 4-0 na Gor Mahia kwenye mchezo uliopigwa dimba la Moi Kasarani Jumatano jioni.
Yanga ilionyesha mchezo mbovu, hakika kipigo hicho hakikuwa cha kushangaza.
Mabao ya Gor Mahia yalifungwa na Tuyisenge, Guikan aliyepachika mabao mawili huku mlinzi Haji Mwinyi akijifunga bao la tatu.
Wachezaji wa Yanga hawakuonekana kuwa mchezoni tangu mchezo huo ulipoanza, Gor Mahia ilitawala kila idara.
Hakika Yanga ina kazi ya ziada kuweza kutengeneza kikosi cha ushindani kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom mwezi ujao.
Ushindi huo unaifanya Gor Mahia ifikishe alama tano na kujiimarisha katika nafasi ya pili kundi D nyuma ya USM Alger ambayo imepata ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Rayon Sports.
Rayon Sports imesalia nafasi ya tatu ikiwa na alama mbili na mabao mawili ya kufunga huku ikifungwa mabao matatu wakati Yanga imeendelea kuburuza mkia ikiwa na alama moja haijafunga bao na imefungwa mabao nane.

ADVERTISE HERE