Zahera kukutana na Kamati ya Usajili Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2018
Zahera kukutana na Kamati ya Usajili Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amepanga kukutana na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika ili kujua maendeleo ya mchakato wa usajili.

Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa wiki ijayo Julai 26, mpaka sasa Yanga ikiwa imesajili wachezaji sita.

Zahera amechukizwa na kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Gor Mahia juzi ambapo jana baada ya Yanga kurejea aliwaambia waandishi wa habari kuwa timu hiyo inahitaji mabadiliko makubwa ya kikosi chake.

"Hapana. Ni lazima tufanye kitu cha maana, ninapaswa kukutana na viongozi wa Kamati ya Usajili, kuna haja ya kukijenga kikosi upya,ΓƒΒ’Γ’β€šΒ¬Γ‚Β Zahera amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti.

"Kwanza nataka wafanye haraka usajili wa wachezaji niliowapendekeza kulingana na maeneo husika, hii itasaidia kuirudisha timu katika hali yake.

"Pia wachezaji muhimu waliomaliza mikataba nao washughulikiwe, wana msaada mkubwa ndani ya timu, sitapenda kusikia wanaondoka.

"Mabadiliko ya timu hasa kwa wachezaji wapya ni muhimu, ni lazima kufanya hivyo haraka, ingawa hawatatumika katika mashindano haya."

Zahera alisema wamepoteza mechi ya Gor Mahia kwa sababu timu haikuwa pamoja kwa muda mrefu.

"Nitawaomba viongozi tusivunje kambi ili tukae pamoja kujenga timu na kurekebisha makosa yaliyojitokeza,ΓƒΒ’Γ’β€šΒ¬Γ‚Β aliongeza Zahera.

Katika hatua nyingine Zahera ametaka wachezaji Mrisho Ngassa, Deus Kaseke na straika Heririer Bakambo masuala yao na CAF yakamilishwe haraka iwezekanavyo.

Katika usajili wa dirisha dogo wa CAF ambao Yanga walitakiwa kuongeza majina matatu, walichelewa kutuma majina hayo kwa sababu kuna mambo hawakukamilisha.

"Naomba viongozi wafanyie kazi hilo kwa haraka kwani tukiwatumia wachezaji hawa katika mechi ijayo na Gor Mahia itakuwa vizuri, wanaweza kuongeza kitu katika timu," alisema.

Yanga itaendelea na program ya mazoezi kesho Jumamosi, baada ya leo baadhi ya wachezaji kushindwa kutokea mazoezini sababu ikielezwa ni uchovu huku wengine wakiwa na madai kwa uongozi wa Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’