Furaha tunaianza rasmi Julai 29 - Ngassa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jul 2018
Furaha tunaianza rasmi Julai 29 - Ngassa
Mmoja wa wachezaji walioongezwa kwenye kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho, Mrisho Ngassa amesema furaha itarejea rasmi Jangwani tarehe 29 Julai 2018 kwenye mchezo dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa dimba la Taifa.

Ngassa, Deus Kaseke na Heritier Makambo majina yao yalitumwa CAF ikiwa ni usajili mpya kwa ajili ya michuano ya kombe la Shirikisho.

Hata hivyo wachezaji hao juzi hawakujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kilicholazwa mabao 4-0 na Gor Mahia sababu ikielezwa kuchelewa kutumwa kwa majina yao CAF.

Imeelezwa tayari CAF imeidhinisha usajili wa wachezaji hao hivyo wanaweza wakatumiwa na Yanga katika mchezo ujao.

Yanga inatarajiwa kuendelea na mazoezi kesho kujiandaa na mchezo huo ambao itahitaji kushinda ili kufufua matumaini ya kutinga robo fainali.

Licha ya kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi D ikiwa na alama moja, Yanga ina michezo miwili ya nyumbani ambayo kama itashinda inaweza kufikisha alama saba kabla ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Rayon Sports ugenini.

Gor Mahia iliyo nafasi ya pili ina alama tano lakini imebakisha mchezo mmoja wa nyumbani dhidi ya Rayon Sports.

Rayons Sports iko nafasi ya tatu ikiwa na alama mbili, ina mchezo mmoja wa nyumbani dhidi ya Yanga.

Gor Mahia na Rayon Sports zote zitasafiri kwenda Algeria kuikabili USM Alger ambayo inaongoza kundi D ikiwa na alama saba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’