Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema klabu hiyo haikupewa mchezaji wa bure na Singida United.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Yanga jijini Dar es salaam, Nyika amesema wachezaji Deus Kaseke na Feisal Salum walisajiliwa kihalali kwa kutumia fedha za Yanga.
Nyika amesema Yanga ilinunua mkataba wa mwaka mmoja wa Deus Kaseke kwa kumlipa fedha za usajili ambazo hazikuwa zimelipwa na Singida United.
Pia Nyika amesema Fei Toto alisajiliwa kihalali na Yanga, walikutana na Singida United kiungwana ili kupata maridhiano baada ya klabu hiyo nayo kutangaza imemsajili.
Lakini Nyika amesisitiza Yanga ilitoa fedha kumnunua mchezaji huyo hivyo sio kweli kwamba wamepewa na Singida United kwa hisani ya Rais wa klabu hiyo Mwigulu Nchemba
Kuhusu beki Elisha Muroiwa, Nyika amesema Yanga ilikataa kumsajili mchezaji huyo baada ya kocha Mkuu Mwinyi Zahera kutorishishwa na kiwango chake.

ADVERTISE HERE