Muujiza umeshindikana kombe la Shirikisho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jul 2018
Muujiza umeshindikana kombe la Shirikisho
Kwenye michuano ya kombe la Shirikisho, katika michezo minne iliyocheza, Yanga imeruhusu mabao 11 huku ikifunga mabao mawili kwenye mchezo wa leo dhidi ya Gor Mahia.

Imeruhusu jumla ya mabao saba dhidi ya Gor Mahia na mabao manne dhidi ya USM Alger. Takwimu hizi sio za kupendeza hata kidogo machoni mwa mashabiki wa Yanga.

Lakini swali la kujiuliza je Yanga ina kikosi imara cha kushindana kwenye michuano ya kombe la Shirikisho? jibu ni HAPANA.

Ni hivi, katika michuano hii wachezaji wenye sifa ya kushiriki ni wale walioitumikia Yanga msimu uliopita ukiongeza wawili (Kaseke na Matheo) waliosajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili wa CAF.

Kikosi cha Yanga kimeathiriwa na kukosa wachezaji wenye uzoefu wa michuano hiyo namba mbili kwa ukubwa barani Afrika katika ngazi ya vilabu.

Nadir Haroub, Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Kelvin Yondani, Fiston Kayembe na Hassani Kessy hawa wote walisajiliwa kwa ajili ya michuano hii.

Yondani, Kamusoko na Tambwe ndio wachezaji ambao bado wako Yanga lakini ni dhahiri hawakuwa 'fit' kuweza kutumika hata kwenye mchezo wa leo dhidi ya Gor Mahia.

Yondani amefanya mazoezi siku mbili tu tangu akamilishe usajili wake huku Kamusoko akichelewa kurejea kutoka Zimbabwe alikokwenda mapumziko.

Licha ya kupona majeraha, Tambwe bado hajaweza kurejesha makali yake.

Yanga inalazimika kushiriki michuano hii kwa kutumia wachezaji waliopo ambao majina yao yalitumwa CAF msimu uliopita.

Kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Gor Mahia kimedhihirisha udhahifu wa kikosi cha Yanga cha michuano ya kombe la Shirikisho.

Michezo miwili iliyobaki ni ya kukamilisha ratia tu, ni vyema Yanga ikajikita zaidi kwenye maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom unaotarajiwa kuanza katika kipindi cha wiki tatu zijazo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’