Yanga kumuongezea Zahera makocha wawili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jul 2018
Yanga kumuongezea Zahera makocha wawili
Katika kuliboresha benchi la ufunsi la Yanga, Mwenyekiti wa kamati ya usajili Hussein Nyika amesema kabla ya ligi kuanza kamati yao imelazimika kuvunja benki kuhakikisha inashusha makocha wawili, mmoja mzawa na mwigine wa kigeni ili kumsaidia Mwinyi Zahera na kuimarisha benchi la ufundi.

Nyika amesema wanataka kumshusha Kocha Msaidizi namba moja wa Zahera ambaye lazima awe mzawa ili kuchukua nafasi ya Shadrack Nsajigwa ambaye mkataba wake ulimalizika.

Awali Yanga ilimpokea Kocha Mkongo Gay Bukasa ambaye aliondoka kimyakimya baada ya kushindwa kufikia makubaliano na uongozi wa yanga.

Kwa muda mrefu Yanga imekuwa ikihusishwa na mpango wa kumpa ajira kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime kuja kusaidiana na Zahera akiambatana na Mzambia Noel Mwandila.

Mbali na kocha huyo pia Nyika alisema wanataka kumalizana haraka na kocha Mkenya wa makipa Razack Siwa ambaye alitua nchini wiki iliyopita anayekuja kuchukua nafasi ya Juma Pondamali.

β€œTunataka kuongeza nguvu katika benchi letu, tunataka pia kuongeza kocha mmoja mzawa atakayeungana na Mwandila kumsaidia kocha Zahera lakini pia tunaona kuna mashaka ya kiufundi katika kocha wa makipa.

β€œKama mlivyoona kwasasa tupo katika mazungumzo ya mwisho na kocha Siwa nafikiri sasa tutamalizana naye ili aje aanze kazi haraka kupandisha viwango vya makipa wetu,” Nyika ameuambia mtandao wa Mwanaspoti.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’