Kaaya afafanua michango ya mashabiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Aug 2018
Kaaya afafanua michango ya mashabiki
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaaya amesema sio dhambi kwa mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuichangia timu yao pale inapokuwa na shida.

Kumekuwa na mijadala miongoni mwa wadau wa soka nchini kufuatia ombi hilo la kuchangiwa klabu ya Yanga lililotolewa na Kaaya juzi.

"Yanga ina changamoto za kiuchumi. Sio vibaya kwa wanachama na mashabiki ambao ndio wenye timu wakiichangia ili kuwezesha kutatua baadhi ya changamoto hizo," amesema.

"Watu wamekuwa wakitafsiri kila mmoja kwa namna anavyoelewa huku wengine wakisema kuwa klabu itatembeza bakuli jambo ambalo si sawa."

"Huu ni utaratibu wa kawaida tu wenye lengo la kuwashirikisha wadau wa klabu ya Yanga kuhusika moja kwa moja kuisaidia timu yao."

Kumekuwa na maoni tofauti juu ya mpango huo wa viongozi wa Yanga ambao baadhi ya wadau wanadhani ni wa muda mfupi na ni vyema Yanga ingekuja na mawazo ya kumaliza kabisa changamoto zake.

Lakini pia wapo miongoni mwao wanaomtupia lawama aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga ambaye tayari amejiuzulu.

Akihojiwa na EFM, Mzee Ibrahim Akilimani amemtupia lawama moja kwa moja Sanga kwamba aliikwamisha Kamati Maalum ya Mpito iliyoundwa na Bodi ya udhamini ya Yanga siku ya Mkutano Mkuu wa Wanachama Juni 10 2018.

Akilimali amesema ni Sanga aliyesababisha Kamati hiyo kuvunjika baada ya kuibadilishia majukumu kinyemela na kuinyima ushirikiano.

Mzee AKilimali ameongeza kuwa iwapo Kamati hiyo ingeachwa ifanye kazi kama ilivyoagizwa siku ya Mkutano Mkuu, leo hii Yanga isingeomba kuchangiwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’