Leo saa saba na nusu mchana uongozi wa klabu ya Yanga utakuwa na mkutana na waandishi wa habari, Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es salaam.
Jana Kamati ya Mashindano chini ya Mwenyekiti wake Hussein Nyika ilifanya kikao kujadili masuala mbalimbali likiwemo la mlinda lango Youthe Rostand ambaye hakusafiri na kikosi cha Yanga kwenda mkoani Morogoro.
Huenda katika Mkutano huo ikatolewa taarifa rasmi juu ya mlinda lango huyo ambaye ni dhahiri hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya msimu ujao.
Yanga kucheza na Mawenzi FC
Wakati huo huo August 12, 2018 klabu ya Yanga itacheza mchezo wa kirafiki na Mawenzi FC katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Mchezo huo utakuwa sehemu ya bonanza ambalo pia litahusisha burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Utakuwa mchezo maalum kumuaga mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' aliyestaafu na kuteuliwa kuwa Meneja wa Yanga.

ADVERTISE HERE