Unakosaje kushuhudia Nadir anavyoagwa August 12 uwanja wa Jamhuri?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Aug 2018
Unakosaje kushuhudia Nadir anavyoagwa August 12 uwanja wa Jamhuri?
Kikosi cha Yanga kiko mkoani Morogoro kikiendelea na maandalizi ya msimu mpya pamoja na michezo iliyobaki ya michuano ya kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger (Aug 19) na Rayon Sports (Aug 28).

Aidha, Yanga inatarajia kumuaga nahodha wake, Nadir Haroub maarufu kama Cannavaro kwa kucheza mchezo wa kirafiki na Mawenzi FC ya Morogoro inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Mchezo huo utachezwa Agosti 12, kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Yanga imeamua kumuaga Cannavaro kwa shamrashamra za aina yake kwani siku hiyo Uwanja wa Jamhuri utakuwa na burudani za kila aina kuanzia asubuhi.

Wasanii wakiwemo mwigizaji Wema Sepetu, Msaga Sumu na Juma Nature wanatarajiwa kuwa sehemu ya Burudani hiyo.

Siku hiyo pia kutakuwa na tukio la uzinduzi rasmi wa timu ya Wanawake ya Yanga itakayofahamika kama Yanga Queens.

Wachezaji wapya kutambulishwa

Yanga itatumia mchezo dhidi ya Mawenzi FC kutambulisha wachezaji wake wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu wa 2018/19.

Klaus Kindoki, Heritier Makambo, Jaffar Mohammed, Mrisho Ngassa, Mohammed Issa 'Banka', Deus Kaseke na fundi Feisal Salum 'Fei Toto' wote wataonekana rasmi dimbani wakianza kuitumikia Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’