Viongozi Yanga wameshindwa kutekeleza agizo la Serikali

Suleiman Sudi By Suleiman Sudi
β€’
8 Aug 2018
Viongozi Yanga wameshindwa kutekeleza agizo la Serikali
Juni 10, 2018 ilikuwa siku ya Mkutano Mkuu wa Wanachama Yanga ambapo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alialikwa kuiwakilisha Serikali kwenye Mkutano huo.

Dk Mwakyembe akautaka uongozi wa Yanga kuhakikisha ndani ya siku 60 uwe umefanya uchaguzi kujaza nafasi zilizo wazi.

Hata hivyo huenda agizo hilo la Serikali likashindwa kutekelezwa kwani zimebaki siku mbili tu siku 60 zitimie pasipo kuwa na mwito wowote kutoka kwa uongozi wa Yanga.

Aidha tangu kutolewa kwa agizo hilo, viongozi zaidi wa Yanga wameendelea kujiuzulu akiwemo aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga na Mjumbe mwingine wa Kamati ya Mashindano.

Kujiuzulu kwa viongozi zaidi kunapaswa kuifanye Yanga ione umuhimu na uharaka wa kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura.

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo wakiutaka uongozi kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura haraka ili kupata viongozi wengine.

Kwa sasa Yanga haina Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti wala Katibu Mkuu.

Nafasi ya Katibu Mkuu inakaimiwa na Omary Kaaya aliyeteuliwa hivi karibuni na Bodi ya Wadhamini ya klabu ya Yanga.

Bado kumekuwa na sintofahamu juu ya hatma ya Yusufu Manji ambaye imeelezwa bado ni Mwenyekiti wa Yanga anayetambuliwa na TFF.

Ni karibu miezi miwili sasa imepita tangu Wanachama wa klabu hiyo waikatae barua yake ya kujiuzulu na kumuomba arejee kwenye nafasi yake, amekuwa kimya.

Kabla ya kujiuzulu, aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga alisema uongozi wa Yanga ulionana na Manji ambaye kimsingi alikubali kurejea lakini akataka apewe hadi miezi mitatu ili aweze kujipanga.

Hata hivyo wengi walitegemea ahadi hiyo ingetolewa na Manji mwenyewe na sio viongozi ambao ilikuwa kawaida yao kumtumia bilionea huyo kuwatuliza wanachama kila mambo yalipokwenda kombo.

Kuna umuhimu mkubwa kwa Yanga kumaliza 'utata' wa uongozi wake kwa kupata viongozi wapya kwani ni hatari timu kukaa muda mrefu bila ya kuwa na viongozi wake waandamizi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’