Nahodha wa muda mrefu zaidi wa kikosi cha Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' ameanza rasmi majukumu yake kama Meneja wa timu.
Nadir aliyeitumikia Yanga kwa miaka 12 ameanza majukumu hayo leo ambapo asubuhi alisimamia mazoezi yanayofanyika kwenye uwanja wa Highland Park mkoani Morogoro akiwa sambamba na benchi la Ufundi.
Nadir amesema ataitumikia Yanga kikamilifu katika nafasi hiyo mpya kama alivyokuwa mchezaji.
Ametaka ushirikiano kutoka kwa WanaYanga ili aweze kufanikiwa katika majukumu hayo.
"Nitakaa na aliyekuwa mtangulizi wangu (Hafidh Saleh) ili anielekeze baadhi ya mambo lakini jambo la muhimu zaidi nahitaji ushirikiano kutoka kwa WanaYanga wote ili niweze kufanikiwa," amesema.
Nadir anatarajiwa kuagwa kwa heshima Jumapili, August 12 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kwa Yanga kucheza na Mawenzi Market.

ADVERTISE HERE