Mshambuliaji mpya wa Yanga Mcongomani Heritier Makambo anaweza kuitumikia Yanga kwenye mchezo ujao wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger baada ya jina lake kuidhinishwa na CAF.
Makambo hakuitumikia Yanga kwenye mchezo uliopita dhidi ya Gor Mahia licha ya jina lake kutumwa CAF sambamba na Matheo Anthony na Deus Kaseke sababu ikielezwa ni kuchelewa kwa mchakato wake wa usajili.
Kaseke na Matheo majina yao yaliidhinidhwa mapema
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaaya amesema mchezaji huyo tayari ameidhinishwa na anaweza kutumika kwenye mchezo dhidi ya USMA na ule unaofuata dhidi ya Rayon Sport.

Kikosi cha Yanga kimeweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na michezo hiyo pamoja na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

ADVERTISE HERE