Yanga yamstaafisha Cannavaro kwa heshima, yaichapa Mawenzi Mareket 1-0

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Aug 2018
Yanga yamstaafisha Cannavaro kwa heshima, yaichapa Mawenzi Mareket 1-0
Yanga imemuaga rasmi nahodha wake wa muda mrefu zaidi Nadir Haroub 'Cannavaro' kwa kuichapa Mawenzi Market bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.

Nadir aliyeitumikia Yanga kwa miaka 12 alipata nafasi ya kucheza kwa dakika 10 kabla ya kumpisha Kelvin Yondani ambaye pia alimkabidhi rasmi kitambaa cha unahodha.



Mkongwe huyo pia alikataa jezi yake namba 23 kustaafishwa licha ya viongozi wa Yanga kupendekeza kusitisha matumizi ya jezi hiyo kwa ajili ya heshima yake.

Badala yake amemrithisha beki Abdallah Shaibu 'Ninja' akiwa na matumaini makubwa kwa chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 kuwa ataweza na hata kuzidi mafanikio yake.



Baada ya tukio hilo lililochukua takribani dakika tano, mchezo uliendelea.

Kikosi cha Yanga kimeonekana kuboreka sana kwenye mchezo huo kwa kutandaza kandanda safi na kuonyesha umakini mkubwa.

Katika kipindi cha kwanza kocha Mwinyi Zahera aliwatumia Abdallah Shaibu, Feisal Salum 'Fei Toto' na Papi Tshishimbi kama viungo na kufanikiwa kutawala sehemu ya kati.

Aidha kiungo Fei Toto ameongeza ubora na ubunifu katika sehemu ya kiungo akionekana kuelewana vyema na Papi Tshishimbi.

Bao pekee la Yanga lilipatikana kwenye kipindi cha pili likiwekwa kimiani ya mshambuliaji mpya Heritier Makambo aliyevunja mtego wa kuotea na kuuwahi mpira wa adhabu uliopigwa na Juma Abdul.

Kwenye kipindi cha pili Yanga iliwaingiza Raphael Daudi, Pius Buswita na Juma Mahadhi nafasi za Abdallah Shaibu, Mrisho Ngassa na Deus Kaseke.

Mabadiliko hayo yaliiongezea Yanga kasi ya mashambulizi na kungekuwa na umakini, pengine mabingwa hao wa Kihistoria Tanzania Bara wangeweza kuibuka na ushindi mnono zaidi.

Kwenye mchezo huo Yanga pia ilimtumia mlinda lango wake mpya Klaus Kindoki ambaye naye ameonyesha kiwango kizuri.

Baada ya mchezo huo, uongozi wa Yanga umekusudia kuwapa nafasi ya kumuaga Nadir wakazi mkoa wa Dar es salaam Jumapili ijayo kwenye mchezo wa kombe la SHirikisho dhidi ya USM Alger.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’