Uongozi wa klabu Yanga umeanza kutoa fomu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali zilizowazi baada ya kujiuzulu kwa waliokuwa viongozi wake.
Juzi Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaaya alisema wameanza mchakato huo na watahakikisha wanaukamilisha kwa wakati.
Wiki iliyopita Shirikisho la soka nchini (TFF) lilitoa siku 75 kwa vilabu vya Yanga na Simba kuhakikisha vimefanya uchaguzi.
Wakati Simba ikiagizwa ifanye uchaguzi wa kupata viongozi wapya, Yanga iliagizwa ifanye uchaguzi kujaza nafasi za viongozi waliojiuzulu.
Viongozi waliojiozulu nafasi zao Yanga ni pamoja Yusuf Manji aliyekuwa Mwenyekiti, Clement Sanga, Makamu Mwenyekiti, Salum Mkemi na Hashim Abdallah waliokuwa kwenye Kamati ya Utendaji.
Awali ilielezwa kuwa Manji alikuwa ameridhia kurejea lakini ukimya wake unaashiria bado hayuko tayari.
Anayepigiwa chapuo na wengi kumrithi Manji ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania SPORTPESA, Tarimba Abbas Tarimba.
Wengine ambao huenda wakaingia katika kinyan'ganyiro cha kuwania nafasi hizo ni pamoja na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Abdalah Bin Kleib na Mbunge wa Iramba Mashariki, Dk. Mwigulu Nchemba.

ADVERTISE HERE