Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa ametoka Hospitalini nchini India baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Mkwasa alisafirishwa kutibiwa nchini India mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kubainika kuwa na matatizo ya moyo yaliyopelekea ajiuzulu wadhifa wake kwenye klabu ya Yanga.
Mkwasa ambaye amewahi kuichezea klabu ya Yanga kwa mafanikio, bado yuko nchini India akiwa chini ya uangalizi wa madaktari kabla ya kuruhusiwa kurejea nchini.
Mke wa mkongwe huyo, Betty Mkwasa amethibitisha mumewe kupewa ruhusa ya kutoka Hospitalini.
“Anaendelea vizuri sana kiafya na sasa ameshatoka hospitali, tupo hotelini licha ya kuwa bado yupo chini ya uangalizi wa daktari Nilesh,” Betty Mkwasa aliliambia gazeti la Championi

ADVERTISE HERE