Subirini ligi ianze - Fei Toto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2018
Subirini ligi ianze - Fei Toto
Kiungo fundi wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' amesema kuwa amejipanga kikamilifu kuisaidia Yanga ili iweze kufanya vizuri msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania Bara unaoanza wiki ijao.

Fei Toto aliyesajiliwa na Yanga kutoka klabu ya JKU amekuwa akionyesha kiwango cha juu katika michezo ya kirafiki aliyocheza.

Kiungo huyo kutoka Zanzibar amejihakikishia namba mapema kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Mwinyi Zahera. Amesema yupo fiti kwa mapambano na viungo wa timu pinzani

"Sipendi kuzungumzia timu moja wakati ligi ina timu 20 natambua Simba ndio wapinzani wetu na ndio timu ambayo imekuwa ikiangaliwa kwa ukaribu zaidi kutokana na kushikilia ubingwa.

"Hivyo nitapambana kuhakikisha nairudisha timu yangu kwenye makali ya misimu mitatu iliyopita kwa kusaidiana na wenzangu," Fei Toto amenukuliwa na Mwanaspoti.

Fei Toto alisema mchezaji yeyote anayejua anachokifanya hawezi kuogopa upinzani hivyo kutokana na uwezo alionao anataka aonyeshe kile anachoamini ndio kitaisaidia Yanga kufanya vizuri kwenye ligi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’