Jana Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yususfu Manji alikutana na wachezaji na viongozi wa Kamati ya Mashindano ya Yanga kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo mpambano wa leo kukamilisha ratiba dhidi ya USM Alger.
Mpema jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Hussein Nyika alisema kamati yake ilifanya kikao na mwenyekiti wao, ambaye alikuwa nje ya soka kwa muda mrefu na amewahakikishia atakuwepo uwanjani hapo leo.
Jana usiku, Manji alipata chakula pamoja na wachezaji na viongozi, pia alizungumza na wachezaji.
βManji ameahidi atakuwepo uwanjani leo hivyo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuiona timu na kumwona kiongozi wao na tuna imani kubwa kufika kwake ni mwanzo mzuri kwetu na baada ya hapo tutafanya mengine zaidi ya kimaendeleo,β alisema Nyika.
Naye Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema kikosi na wachezaji wote ambao wana leseni ya kushiriki mashindano hayo wapo fiti na jukumu litabaki kwa Zahera kuamua nani wa kumtumia katika mechi hii.
Ten alisema viingilio vitakuwa Sh3,000, kwa mzunguko VIP B na C itakuwa Sh7,000 wakati VIP A itakuwa Sh10,000 na tuna imani viingilio rahisi kwa kila mpenzi wa soka kuja kushuhudia burudani.
βMgeni rasmi kama kawaida atakuwa Jenerali Venance Mabeyo, pia tulimwalika Rais wetu John Pombe Magufuli, ambaye amekuwa akitupa ushirikiano wa kutosha, lakini hataweza kuhudhulia kutokana kuwa na majukumu mengine ya kitaifa,β alisema Ten.
Yanga imepata mzuka huo ikiwa pia inajiandaa na michuano ya Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza Agosti 22 na itaanza kukipiga na mabingwa wa kombe la FA, Mtibwa Sugar ya Morogoro, August 23 kwenye uwanja wa Uhuru.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE