Moja ya mambo ambayo Yanga imekuwa ikifanikiwa katika usajili wake, ni kuibuka na wachezaji ambao awali majina yao yanakuwa hayafahamiki lakini wanakuwa wakali.
Usajili uliowahusisha Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Papi Tshishimbi na sasa Heritier Makambo, unadhihirisha ubora wa 'scouting' inayofanywa na Yanga.
Kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji Heritier Makambo kwenye mchezo dhidi ya USM Alger, kinadhihirisha kuwa Yanga inajua kutambua wachezaji wazuri.
Makambo ameonyesha kuwa na vitu vingi, ingawa bado ni mapema, lakini unaweza kutabiri kuwa atafunga mabao mengi sana kama hatakumbwa na majeruhi ya mara kwa mara.
Uwezo wake unatukumbusha msimu wa kwanza wa Donald Ngoma alipojiunga na Yanga.
Leo hii pengine waarabu wamejuta kukutana na McongoMan huyo ambaye ujio wake umefanikishwa na kocha Mwinyi Zahera.

ADVERTISE HERE