Leo tunaanza upyaaa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Aug 2018
Leo tunaanza upyaaa
Ndio neno unaloweza kulitumia leo ambapo ligi kuu ya Tanzania Bara inaanza kwa vumbi kutimkia katika viwanja sita tofauti.

Msimu huu ligi inatarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake kutokana na maandalizi yaliyofanywa na kila timu.

Lakini pia ongezeko la timu kutoka 16 hadi 20 litaongeza msisimko.

Yanga yenye Historia ya kutwaa taji hilo mara 27 itaanza kampeni ya kurejesha ubingwa wake kesho Alhamisi saa 12 jioni itakapochuana na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Taifa.

Yanga iliyokuwa imeweka kambi ya wiki mbili mkoani Morogoro imerejea na nguvu mpya juzi ikiichapa USM Alger mabao 2-1 kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho.

Yanga, Simba na Azam FC zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali kwenye mbio za ubingwa huku Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar, Singida United na KMC zikiwa hazitabiriki.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mafanikio ya kikosi chake msimu huu yatategemea utimamu wa afya wa wachezaji wake.

Msimu uliopita Yanga iliathiriwa sana na majeruhi ya mara kwa mara ya wachezaji wake waandamizi.

Kuna wakati wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza walikuwa majeruhi. Yanga ililazimika kushiriki mashindano mengi ikiwa na kikosi 'finyu'.

Zahera amesema hapendi kuliona hilo likitokea msimu huu. Amesema atahakikisha angalau asilimia 80 ya wachezaji wanakuwa na utimamu wa kimwili.

Mcongoman huyo ametamba kuwa na kikosi kipana ambacho anaamini kitaweza kutwaa ubingwa msimu huu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’