Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeanza leo ambapo michezo mitano tayari imepigwa katika viwanja mbalimbali.
Mkoani Mwanza, Mbao FC imeanza vyema ligi hiyo baada ya kuwalaza ndugu zao kutoka jijini humo Alliance kwa bao 1-0.
Kule mkoani Singida, wenyeji Singida United wameonja joto ya jiwe baada ya kulazwa kwa bao 1-0 na timu iliyopanda daraja, Biashara FC.
Kule Tanga, Coastal Union ikalazimishwa sare ya bao 1-1 na Lipuli FC. Wakati kule mkoani Kagera, wenyeji Kagera Sugar wamepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.
Ruvu Shooting ya Masau Bwire 'imepapaswa' na Ndanda FC baada ya kuchapwa 1-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Mabatini, Ruvu.
Simba na Prisons zitachuana kwenye mchezo unaotarajiwa kuanza saa mbili kamili usiku.

ADVERTISE HERE