Mziki wa Tshishimbi, Fei Toto alivyowatesa viungo Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2018
Mziki wa Tshishimbi, Fei Toto alivyowatesa viungo Mtibwa Sugar
Viungo wa Yanga, Papy Tshishimbi na Feisal Salum kombinesheni yao imekuwa gumzo katika uwanja wa Taifa kwa jinsi walivyocheza leo.

Feisal na Tshishimbi katika kipindi cha kwanza walikuwa wakicheza huru baada ya Abdallah Shaibu 'Ninja' kuwakabia na waliweza kutawala dimba la katikati.

Ninja kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha viungo Shaban Nditi na Awadh Juma wanakuwa hawachezi kwa wepesi katika eneo hilo.

Mabadiliko yalipofanyika baada ya Ninja kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Ajib, Yanga walizidi kucheza katikati.

Feisal na Tshishimbi pamoja na Ajib walikuwa wakicheza wote na kusambaza mipira kwa pamoja hali iliyowafanya Mtibwa wapate tabu.

Mtibwa walifanya mabadiliko ya kumtoa Awadh Juma na nafasi yake kuchukuliwa na Ally Makalani, mabadiliko ambayo yalionyesha kuwa na tija kwa Mtibwa kwani waliamka na kuanza kucheza mpira.

Mabadiliko hayo yaliisaidia Mtibwa kupata bao kupitia kwa Haroun Chanongo, ambaye nae aliingia kuchukua nafasi ya Salum Kihimbwa.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
23m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’