Wakati akitangaza bao la kwanza la Yanga kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa SUgar jana lililofungwa na mshambuliaji Heritier Makambo, mtangazaji wa kituo cha runinga cha Azam, Baraka Mpenja alitumia jina la Makambovic kusherehesha bao hilo alilofunga kwa kichwa kwenye dakika ya 31 ya mchezo.
Makambo ameonesha kulifurahia jina hilo alilobatizwa na Mpenja hivyo kulifanya kuwa jina lake la utani 'aka Makambovic'.
"Nimelikubali jina hili la Makambovic. Nimeikubali kazi yako Baraka Mpenja, " ameandika Makambo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
Makambo ameanza vyema maisha yake ya soka katika klabu ya Yanga akifanikiwa kutupia mabao mawili katika michezo miwili iliyopita.

ADVERTISE HERE