Yanga kuongeza mshambuliaji dirisha dogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Aug 2018
Yanga kuongeza mshambuliaji dirisha dogo
Licha ya Heritier Makambo kuanza vyema kuitumikia Yanga, kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Kihistoria Mwinyi Zahera amesema timu hiyo itasajili mshambuliaji mwingine dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwezi Novemba.

Yanga ilifanikiwa kusajili mshambuliaji mmoja pekee wakati wa dirisha kubwa la usajili kutokana na kukumbwa na changamoto za kiuchumi.

Zahera amesema Yanga haiwezi kumtegemea Makambo peke yake kwenye safu ya ushambuliaji, ni lazima apate mtu wa kusaidiana nae.

"Nilipendekeza apatikane mshambuliaji wa kusaidiana na Makambo pamoja na mlinzi wa kulia wa kushirikiana na Juma Abdul," amesema Zahera.

"Yanga inao washambuliaji wengi, lakini tunahitaji mshambuliaji mwingine mwenye uwezo sawa au zaidi ya Makambo"

"Kwa sasa timu yetu imekamilika kwa kuwa na mchezaji zaidi ya mmoja katika kila nafasi isipokuwa namba mbili na namba tisa kwa maana ya ushindani kati ya wachezaji waliopo.

"Tunahitaji kuimarisha kikosi chetu kwa kuongeza nguvu nafasi hizo kwa kusajili wachezaji wenye uwezo sawa au zaidi ya waliopo ili kuongeza ushindani."

Wakati Amissi Tambwe, Yohana Mkomola na Matheo Anthony wanaweza kucheza namba tisa ikitokea Makambo hayupo, Yanga inakabiliwa na mtihani zaidi kwenye nafasi ya beki wa kulia kama Juma Abdul atakosekana.

Baada ya kushindwa kufikia makubaliano na beki Hassani Ramadhani Kessy aliyetimkia Nkana FC ya Zambia, Yanga haikusajili mbadala wake.

Mchezaji ambaye anaweza kucheza namba mbili ni beki Andrew Vicent ambaye kwa nyakati tofauti wakati yuko Mtibwa Sugar alitumika kwenye nafasi hiyo.

Dirisha la usajili la wachezaji wa kigeni bado liko wazi litafungwa Septemba 06. Hata hivyo TFF imefafanua kuwa muda huo wa ziada umetolewa kwa ajili ya michakato ya kupata vibali na ITC kwa wachezaji ambao walisajiliwa kabla ya Julai 26
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’