Katika mchezo wa juzi dhidi ya Mtibwa Sugar, pasi za mabao mawili ya Yanga zilianzia kwa kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib aliyeingia mapema kwenye kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Abdallah Shaibu aliyeumia.
Kuingia kwa Ajib kuliifanya Yanga iimarike zaidi katika sehemu ya kiungo huku abunifu wake ukiongeza kasi ya mashambulizi.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema Ajib ana kipaji cha hali ya juu lakini kuna mambo machache ambayo yanamfanya asicheze kufikia kiwango chake.
"Wachezaji wote ni wazuri lakini Ajibu anakitu cha ziada, ni mchezaji mwenye akili ya mpira lakini hajijui, anakaa na dhahabu miguuni mwake," Zahera aliuambia mtandao wa ShaffihDauda baada ya mchezo wa juzi
"Nitaendelea kumuimarisha ili aweze kuwa mchezaji bora zaidi"
Ajib alianza kwa kasi kubwa alipojiunga Yanga msimu uliopita hata hivyo kasi hiyo ilipungua baadae kutokana na kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo majeruhi.
Zahera amekuwa akimpa program maalum za mazoezi ya peke yake ili kuhakikisha kipaji chake kinainufaisha Yanga na hata yeye mwenyewe kwani anaweza kupata nafasi ya kwenda kusakata kabumbu nje ya nchi.

ADVERTISE HERE