Niyonzima ameikumbuka Yanga!

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Aug 2018
Niyonzima ameikumbuka Yanga!
Haruna Niyonzima anakiri kwa sasa hana furaha ndani ya Simba kwa vile hachezi, ila anafichua pia hakuondoka Jangwani kwa ugomvi hivyo kama klabu yake hiyo ya zamani itamtaka hana noma kurejea tena kikosini kupiga mzigo.

Kiungo huyo fundi alisema kilichomuondoa Yanga ni kushindwana masilahi, lakini hata leo wakitaka kumrejesha kwa kile alichokuwa akikitaka hana kinyongo kutua Jangwani kwani ni klabu anayoiheshimu na aliyoitumikia kwa mafanikio.

Niyonzima alijiunga Simba msimu uliopita akitokea Yanga mara baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya na klabu yake ya zamani na kufanya maamuzi ya kujiunga na timu hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Haruna alisema Yanga amecheza kwa mafanikio makubwa na ndio timu aliyocheza misimu mingi zaidi anaiheshimu na anaamini sikuikitokea nafasi ya kucheza tena anaweza kufanya ivyo kwasababu hakuondoka kwa ugomvi.

"Kwasasa ni mchezaji wa Simba kwa sababu nina mkataba nao lakini pia naiheshimu Yanga kwasababu imenipa mafanikio makubwa siwezi nikasema Simba nimefika na ndio nitakapomalizia maisha yangu ya soka lakini kwa upande wa Tanzania kama ntashindwa maisha ya Simba na nikapata nafasi timu nyingiune basi iwe ni Yanga,"alisema.

Niyonzima alisema mpira ndio maisha yake hivyo hawezi kuchagua timu ya kucheza kambi ni popote kikubwa anachokiangalia ni pesa na aliweka wazi kuwa alikuwa anatamani sana kubaki Jangwali lakini kutokana na kushindwa kufikia makubaliano ndio sababu iliyomuondoa kikosini hapo.

"Yanga wangenipa pesa niliyokuwa nahitaji sizani kama ningekuwa Simba nipo hapa kwasababu tulifikia makubaliano japo kuna baadhi ya matatizo yaliyopo baina yangu na uongozi yanayonifanya nisicheze ila mimi ni mchezaji wa Simba," alisema.

"Sina maisha ya furaha katika timu yangu kwa sababu sipati nafasi ya kucheza tofauti na maisha niliyokuwa nayo Yanga, nilikuwa na furaha kwasababu nilikuwa muhimu katika kikosi cha kwanza nilikuwa nacheza dakika zote ninazotakiwa kucheza siwezi nikasema ninamaisha mazuri Simba wakati sipati nafasi ya kucheza," alisema.

Niyonzima aliweka wazi kuwa yeye ni mchezaji wa Simba lakini hayupo katika kikosi cha wachezaji wa timu hiyo kutokana na matatizo yaliyopo baina yake na uongozi ambayo hakutaka kuyaweka wazi.

Alisema hawezi kuweka wazi tatizo hilo litabaki kuwa siri yake yeye na uongozi huku akiongeza kuwa ndio sababu iliyomfanya aweze kuchelewa kujiunga na timu na kuongeza kuwa hatua ya mazungumzo kuhusiana na tatizo hilo limefika sehemu nzuri muda wowote watakapolikamilisha atajiunga na timu.

"Najua kuna mashabiki wamenimisi na wanatamani kuniona nikicheza napenda kuwaambia kuwa wataniona saizi wasubili nimalizane na uongozi mambo yakiwasawa nitacheza," alisema Niyonzima.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’