Mlinzi wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael amesema wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Rayon Sports.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo huo, Gadiel amesema wako timamu kimwili na kiakili tayari kwa mchezo huo utakaopigwa saa kumi jioni.
"Tupo sawa kiakili na kimwili tumejiandaa vyema na tupo tayari kwa mapambano tunatambua tupo ugenini na tunacheza na timu bora pia tunaiheshimu."
Naye kocha Mkuu wa Yanga Miwnyi Zahera amesema wanatambua uwezo wa wapinzani ambao watakuwa wanacheza kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Lakini hilo haliwazuia kuondoka na alama zote tatu kwenye mchezo huo.
"Tupo ugenini na tunaheshimu sana wapinzani wetu lakini kikubwa ni kwamba tutaendeleza wimbi letu la ushindi bila kujali tunacheza ugenini au nyumbani au tunacheza na nani," amesema Zahera.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo bila ya kuwa na presha kubwa tofauti na wenyeji wao Rayon wanaosaka ushindi ili kuwania nafasi ya kutinga robo fainali.

ADVERTISE HERE