FT : Yanga 0-1 Ruvu Shooting

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
13 Aug 2017
FT : Yanga 0-1 Ruvu Shooting
Yanga leo imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kulazwa bao 1-0, mchezo huo ukipigwa kwenye dimba la Chamazi linalomilikiwa na Azam FC.

Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika kwenye dimba la Taifa lakini jana yalifanyika mabadiliko baada ya Serikali kuzuia matumizi ya uwanja huo kwa vile ulihitajika kwa ajili ya shughuli ya kiserikali.



Mchezo huo uliokuwa na ushindani kutoka kila upande ulishuhudia mlinzi wa kati Abdallah Shaibu 'Ninja' akijifunga bao pekee la Ruvu Shooting wakati akijaribu kuondosha majaro iliyomiminwa kutoka upande wa kushoto.

Kikosi cha Yanga leo kimecheza vizuri zaidi licha ya kupoteza mchezo ukilinganisha na mchezo wa kwanza dhidi ya Singida United ambapo Yanga ilishinda mabao 3-2

Yanga itaondoka kesho Jumapili asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar ambapo saa moja jioni itacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Mlandege.

Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea kisiwa cha Pemba kuweka kambi kwa ajili ya mchezo wa ngao ya Jamii dhidi ya Simba, August 23.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’