Yanga yaishukuru TFF, yasisitiza Manji amerejea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Aug 2018
Yanga yaishukuru TFF, yasisitiza Manji amerejea
Jana Katibu Mkuu wa Matawi klabu ya Yanga, Boza Kupilika alitoa shukrani kwa TFF kwa ushirikiano waliotoa mpaka Yanga kufanikiwa kukamilisha ushiriki wake kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Boza alisema kuwa wametambua jitihada zilizofanyika kutoka TFF kuhakikisha Yanga wanashiriki vyema mashindano ya kimataifa licha ya kuwa na hali ngumu kiuchumi.

Katika hatua nyingine Boza alisema Mwenyekiti wa Yanga, Yusufu Manji amerejea klabuni hapo na tayari anatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Yanga.

"Mwenyekiti ndiye aliyesaini barua ya shukurani kwa mkuu wa majeshi kwa kuhudhuria mechi ya kombe la shirikisho dhidi ya USM Alger na pia barua ya pole kwa Mheshimiwa Rais kwa kufiwa na Dada yake," alisema Boza.

Mtendaji huyo wa Matawi ya klabu ya Yanga Tanzania amewataka wanachama waendelee kuwa watulivu na amani kwani uongozi upo na unafanya kazi kuhakikisha kila kitu kinafanyika kadri kinavyohitajika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
39m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’