Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mohammed Issa 'Banka' aliyesajiliwa na mabingwa hao wa Kihistoria kutoka klabu ya Mtibwa Sugar bado ni majeruhi.
Banka aliyeshindwa kuitumikia Yanga tangu asajiliwe mwezi Julai, amefichua kuwa anasumbuliwa na tatizo la goti.
"Nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la goti. Tayari nimeshatibiwa na sasa linaendelea kupona."
"Nitaanza kuitumikia Yanga mara tu nitakapokuwa nimepona kabisa na daktari kuniruhusu nirejee dimbani," amesema Banka.
Banka ni mchezaji pekee mpya ambaye bado hajaonekana dimbani (hata mazoezini) kuitumikia Yanga.
Ni miongoni mwa wachezaji saba waliosajiliwa msimu huu.
Wengine ni Klaus Kindoki, Heritier Makambo, Jaffar Mohammed, Mrisho Ngasa, Deus Kaseke na Feisal Salum.

ADVERTISE HERE