Mbao FC inaonekana kuimarika msimu huu baada ya leo kulazimisha suluhu ya bila kufungana dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara raundi ya tatu uliopigwa dimba la Namfua, Singida.
Mbao FC iko kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama saba, ikiwa imeshinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja.
Ligi hiyo itaendelea kesho Jumamosi, Septemba mosi kwa michezo mitano kupigwa kama inavyoonekana hapa chini;
Stand United vs Bishara
Coastal Union vs KMC
Mtibwa Sugar vs Mbeya City
Kagera Sugar vs African Lyon
Prisons vs Alliance
Baada ya michezo ya wikiendi hii, ligi itasimama kwa muda wa wiki mbili kupisha michezo ya Kimataifa kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.
Yanga, Azam FC na Simba michezo yao iliahirishwa kutokana na kutoa wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa 'Taifa Stars'.
Hata hivyo wachezaji wa Simba isipokuwa mlinda lango Aishi Manula, waliondolewa kikosi cha Stars baada ya kuchelewa kuripoti kambini.
Pia yumo kiungo wa Yanga Feisal Salum ambaye naye alichelewa kuripoti kambini mwenyewe akitaja sababu kuwa ni kutokana na kuuguliwa na Baba yake visiwani Zanzibar.

ADVERTISE HERE